• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Baraza La Madiwani Halmashauri ya Mji Njombe Lajadili Taarifa ya CAG

Tarehe iliyowekwa: June 6th, 2020

Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa Mwaka 2018/2019 Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Dorcas Mkello amesema kuwa Halmashauri ilipata Hati inayoridhisha (Hati Safi) yenye masuala mawili ya msisitizo ambapo moja ni miradi ya maji kuhamia Ruwasa na pili ikiwa ni kesi za madai yenye kiasi cha Tshs. 215,384,844 ambapo kama uamuzi utatoka juu ya walalamikaji Halmashauri itatakiwa kulipa fedha hizo.

Wakitoa mapendekezo yao wakati wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa hoja ambazo hazikufungwa baadhi ya Madiwani George Sanga na Sigrada Mligo wamesema kuwa msisitizo uliotolewa kwenye kesi za madai ni vyema Halmashauri ikaona uwezekano wa kufanya majadiliano na walalamikaji nje ya mahakama ili kuweza kupunguza gharama na usumbufu ambao Halmashauri inaweza kuingia kwenye kuendesha kesi hizo.

Kuhusu suala la upungufu wa Watumishi 996 ikiwa ni miongoni mwa hoja zilizojadiliwa jambo linalozuia utendaji kazi za kila siku, Baraza limeshauri Halmashauri kuendelea kuomba na kufuatilia kibali cha kuajiri Watumishi wapya na kutenga bajeti ya mishahara yao licha ya kuwa halipo katika ngazi ya Halmashauri.

Hoja nyingine iliyojadiliwa ni Usimamizi wa Mapato yaliyokusanywa kupitia mashine za kukusanyia mapato (POS) yasiyopelekwa Benki ambapo kiasi cha Tshs. 24,562,752 ziliweza kubainika na Baraza limeshauri kuwa fedha za mapato zikiwa zinakusanywa  ziwe zinawekwa benki au kwa wakala siku zilizokusanywa na ufuatiliaji wa mara kwa mara ufanyike kwenye mfumo ili wakusanyaji wasikae na fedha kwa muda mrefu.

Aidha kwa wale wote waliotumia fedha za makusanyo kinyume na utaratibu Halmashauri ihakikishe kuwa wahusika wote wanarejesha fedha hizo wanazodaiwa. Kwa upande wa Halmashauri kiasi cha Tsh. 17.345,050 zimeshapokelewa kushirikiana na polisi na Halmashauri imeanza kuzuia mishahara yao kuanzia mwezi uliopita kufidia madeni yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri ameipongeza Halmashauri kwa kazi kubwa iliyofanyika mpaka kupelekea hati safi na ameitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa inazuia uwepo wa hoja za ukaguzi kwani nyingine hazina ulazima wa kuwepo.

“Kuna idadi kubwa ya hoja ambazo zinaepukika kama hoja za bima za pikipiki na magari. Kuhusu mikopo na marejesho ya vikundi naungana na serikali mikopo hii kutokuwa na riba. Ni vyema Idara ya Maendeleo ya Jamii iendelee kutoa elimu zaidi na ikaona utaratibu mzuri kuunda vikundi vyenye miradi mikubwa ya pamoja. Tuache kuona mikopo hii kama ni ya kisiasa bali ni kwa ajili ya kuwainua Wananchi wenye kipato cha chini.”Alisema Mkuu wa Wilaya

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Katarina Tengia amelipongeza Baraza kwa usimamizi mzuri kwa kupata hata safi kwa miaka 4 mfululizo na ukusanyaji wa mapato uliovuka lengo.

“Mmefanikisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo katika sekta ya Afya, Ujenzi wa Soko na Stendi Mpya ya kisasa bila kuwa na hoja. Naomba nitoe rai kwa Halmashauri kuhakikisha inaendelea kusimamia udhibiti wa mapato kulingana na uwezo mkubwa wa Halmashauri ulionao katika ukusanyaji mapato ili wakusanyaji wasiweze kuingia kwenye mitego na tamaa. Aidha Halmashauri iendelee kuhakikisha kuwa inajibu hoja zote kwa wakati na kusiwe na hoja za kujirudia katika kaguzi zijazo. Niwaombe kutumia kaguzi za ndani kama jicho la kutabiri kaguzi za mwisho.”Alisema Katibu Tawala

Katika mwaka 2018/2019 kulingana na ripoti Halmashauri ilikuwa na jumla ya hoja 42 kati ya hizo 15 ni hoja za nyuma na 27 hoja za mwaka husika.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe