Baraza la waheshimiwa madiwani Halmashauri ya Mji Njombe kwapamoja waridhia kutenga maeneo ya kujenga Chuo Kikuu.
Wakizungumza madiwani hao katika Mkutano wa baraza la Madiwani Mhe.Ulriki Msemwa ,Honolatus Mgaya ,Mhe.Alatanga Nyagawa , Mhe .Anjela Mwangeni pamoja na wengine walio kuwepo katika baraza hilo wameonesha kiuyao ya kutaka kujengwa kwa chuo kikuu ambacho kitapanua biashara za wananchi na kipato kuongeze .
Aidha akitilia msisitizo wa jambo hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Njombe Mhe.Erasto Mpete amesema jitihada mbalimbali za hukakikisha halmashauri ya mji njombe inakuwa manispa nikuhakikisha vyuo vikuu na vya kati vinajengwa.
"Mkutano huu wa baraza tumeidhinisha kwa pamoja kutenga maeneo ya ujenzi wa chuo kikuu na vyuo vya kati kwa kuwa ajenda ya manispaa ni ya kimkoa ,tunaamini chuo kikuu kinajengwa ndani ya halmashauri ya mji Njombe ili lengo la kuelekea kuwa manispaa liweze kutimia ikiwa ni moja ya vigezo halmashauri kuwa manispaa"
Mhe.Erasto Mpete Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Amos Luhamba Afisa Aridhi Halmashauri ya mji njombe kwaniaba ya Mkurugenzi amesema maeneo ya kujenga chuo kikuu tayari yashatengwa ambayo ni Nundu,Uwemba,Ihalula, na eneo lililokaribu na Shule ya Sekondari Njombe (NJOSS)
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe