Halmashauri ya Mji Njombe leo imefanya uzinduzi wa Baraza la Watoto la Halmashauri linalojumuisha wawakilisha wawili wa Watoto katika kila Kata ya Halmashauri ambapo malengo makuu ya baraza hilo ikiwa ni kupigania haki za watoto na kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto katika Halmashauri ambapo watoto hao wamejumuishwa na wanafunzi kutoka katika shule za Msingi na Sekondari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa baraza hilo Afisa Maendleo wa Halmashauri Bi. Enembora alisema kuwa matamanio yake kwa kipindi kurefu iliku ni kufanikisha uanzishwaji wa baraza la Watoto la Halmashauri ila changamoto kubwa iliyokuwa inawapeleka wao kushindwa kuanzishwa ilikua ni uhaba wa fedha kutokana na kukosa wadhamini na vipaumbele mbalimbali vya Halmashauri lakini kutokana na mipango ambayo Halmashauri imekua ikijiweka katika kila mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha unaoishia 2021/2022 Halmashauri iliona ni vyema kutenga bajeti kupitia mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwezesha uanzishaji na uendelezaji wa mabaraza haya kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka kufikia ngazi ya vijiji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga amesema kuwa zipo haki za msingi za mtoto zinazowawezesha watoto kujumuika, kushiriki, kushirikishwa, kutoa maoni yao kusikilizwa na kufanyiwa kazi katika mikataba mbalimbali ya Kimataifa.“Yapo matukio ya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za watoto katika Halmashauri. Hivyo, nitoe wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanazilinda na kuzihuisha tunu na haki za watoto. Aidha suala la adhabu kwa watoto lazima tufike mahali tuliangalie vizuri. Inafika wakati mtoto anapewa adhabu zilizokidhiri matakwa ya sheria jambo ambalo sio jema. Niwaombe waratibu elimu Kata tukalizingatie hilo.”Alisema Luoga
Aidha amewataka Watoto kuripoti matukio yanayokiuka haki za watoto na kuzitolea haki za watoto kwa mlezi aliye karibu nawe na unayemwamini au kupiga simu namba 116 kupata msaada zaidi ili watoto waendelee kuwa katika mazingira huru na yenye furaha na amani kwa kupata haki za msingi. Thadei amewataka Wazazi na Walezi kuimarisha upendo na umoja kwani familia ndio msingi Mkuu wa malezi ya Mtoto kwenye jamii.na amewataka Watoto kuheshimiana,kupendana na kuthaminiana.
Katika hatua nyingine ya uundwaji wa baraza hilo wawakilishi hao pia walishiriki katika uchaguzi wa viongozi wa Baraza kwa kumchagua Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,Mtunza hazina na Wajumbe Watano ambapo Bernadetha Ramadhan Chibuma kutoka Shule ya Msingi Ramadhani alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la Watoto Halmashauri ya Mji Njombe na kuahidi kuhakikisha kuwa atasimamia kikamilifu utekelezaji wa haki za watoto ndani ya Halmashauri.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe