Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ndugu Judica Omari Novemba 23,2023 ,amefanya ufunguzi wa semina kwa watumishi wa umma Mkoani Njombe juu ya uwekezaji kwenye dhamana za serikali inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mbeya.
Bi Judica amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka huku akiwataka washiriki kusikiliza kwa makini mafunzo hayo muhimu ambayo yatakuwa msaada kwa watumishi na serikali kwa kuwa uwekezaji kwenye dhamana za serikali ni salama na wenye faida kubwa kwa mwekezaji na kwa serikali kwa kuiwezesha kupata mapato.
Akizungumza wakati wa mafunzo Meneja fedha na Utawala kutoka BOT Tawi la Mbeya Bw. Agathon Kipandula, amesema semina hii ni mahususi kwa watumishi kuwahamasisha kuwekeza kwenye dhamana za Serikali. Aidha amesisitiza kuwa Uwekezaji huo ni salama na wenye faida kubwa hivyo watumishi watumie fursa hiyo kufanya Uwekezaji kidogo kidogo ili kuisaidia serikali kwenye mapato na kutekeleza majukumu kwa Maendeleo.
Benki kuu ya Tanzania kwa niaba ya serikali huuza dhamana za serikali ikiwa ni njia mojawapo ya kukopa fedha kutoka soko la ndani kwa makundi mawili ,dhamana za serikali za muda mfupi (Treasury bills) na dhamana za serikali za muda mrefu (Treasury bonds) ambazo huuzwa kwa njia yakufanya mnada kulingana na mpango wa ukopaji wa serikali kutoka masoko ya mahitaji ya ndani ya nchi, bila kuathiri mikopo kwa sekta binafsi.
Benki kuu ya Tanzania (BOT) ni benki ya Serikali yenye wajibu wakutunza fedha zote za serikali ,kukusanya mapato yote yatokanayo na dhamana za serikali na hati fungani pamoja na kulipa wadai na wawekezaji wote wa dhamana na hati fungani pia inazitumia dhamana za serikali na hati fungani kuleta uwiano kwenye ukwasi na ujazi wa fedha nchini Tanzania kama sehemu ya utekelezaji wa sera ya fedha.
Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Halmashauri zote sita zinazounda mkoa wa Njombe wameshiriki semina hiyo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe