• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Bilioni 1.2 zatolewa tamasha la Njombe ya Mama Samia

Tarehe iliyowekwa: November 15th, 2021

Halmashauri ya Mji Njombe imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 kwa vikundi 116 vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu makabidhiano yaliyofanyika katika Uzinduzi wa Tamasha lijulikanalo kama Njombe ya mama samia lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa lengo kuu ikiwa ni  kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo na  pia Wilaya kusogeza huduma karibu na Wananchi kwa kutatua kero zikiwemo ardhi na mirathi.

“Tamasha hili litakuwa kwa muda wa siku tatu lengo kuu ikiwa ni kumshukuru Mheshimiwa Rais kwani kwa kipindi cha muda mfupi na nje ya bajeti Wilaya ya Njombe tumepokea kiasi cha shilingi Bilioni 2.8 fedha za UVIKO na Shilingi Milioni 825 ikiwa ni fedha za tozo. Mheshimiwa Rais alituelekeza sisi viongozi kuhakikisha kuwa tunatatua kero za Wananchi. Tutakuwa na jopo la Wanasheria zaidi ya 20 kusikiliza na kutatua kero za Wananchi,”Alisema Mkuu wa Wilaya

Aliendelea kusema;Kupitia tamasha hili pia Halmashauri ya Mji Njombe inatoa hamasa kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu kunufaika kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya Wanawake .Vijana na Watu wenye Ulemavu nah ii ikawe chachu kwa jamii kujiunga kwenye vikundi na kufanya shughuli za kiuchumi ili kuweza kunufaika na fursa hizo

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hizo kwenye Tamasha la Mama Samia, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya amewataka Wananchi katika maeneo inakotekelezwa miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanashiriki ipasavyo katika kulinda na kutoa taarifa zenye viashiria vya wizi na amewataka Wafanyabiashara kuleta vifaa vyenye ubora unaotakiwa na kutopandisha bei bila sababu ya Msingi jambo ambalo linaweza kupelekea kutokamilika kwa miradi kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.aliendelea kusisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuvumilia yeyote atakayeshiriki kutumia vibaya fedha hizo zilizoelekezwa kwenye miradi hiyo ya afya na elimu.

 “Wito wangu kwa wanavikundi waliopokea fedha hizo kuhakikisha kuwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuinua hali ya uchumi ya Wanakikundi na kuhakikisha kuwa wote waliopokea wanawajibu wa Msingi wa kurejesha ili na wengine wapate fursa ya kukopa. Dawa ya deni ni kulipa. Alisema Mkuu wa Mkoa

Katika hatua nyingine hamasa imeendelea kutolewa kwa jamii  kwa kuchukua tahadhari na kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 na kuhamasisha Wananchi ambao hawajachanja kwenda kuchanja na kutosikiliza upotoshaji kwa ambao hawajachanja ambapo kwa upande wa Halmashauri ya Mji Njombe Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Erasto Mpete aliongoza zoezi la chanjo kwa kuchanja na kudhihirisha kuwa zoezi hilo la uchanjaji ni endelevu kwa ambao hawajachanja.

Tamasha hilo linalofanyika kwa muda wa siku tatu katika viwanja vya stendi ya zamani Njombe na kushereheshwa na wasanii mbalimbali lenye kauli mbiu ya Njombe ya Mama Samia ni la kipekee na Wananchi wemempongeza Mkuu wa Wilaya  na Ofisi yake kwa uratibu wa Tamasha hilo kwani licha ya kutatua kero na kusogeza huduma karibu na Wananchi pia litasaidia kuiweka Njombe kwenye uso wa dunia.

                                                                                                                  

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe