Tarehe 5 Januari 2025, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, amekabidhi hundi mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 ikiwa ni fedha zilizotolewa mkopo kwa vikundi 111 vya wanawake, vijana, na wenye ulemavu katika Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Fedha hizo zimetolewa kama mikopo kwa vikundi vilivyokidhi vigezo vya upatikanaji wa mikopo hiyo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuwawezesha kiuchumi makundi hayo. Kati ya vikundi vilivyonufaika, vikundi 63 ni vya wanawake, 39 vya vijana, na 9 vya watu wenye ulemavu.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Sweda aliwataka wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuimarisha shughuli zao za kiuchumi na kukuza maendeleo ya jamii.
“Malengo ya Serikali ni mazuri,ukitaka matanuzi na fedha ya mkopo wafa,lazima ujue kuweka akiba na mfanyabiashara mzuri anakula kwenye faida ,tuangalie sana kusudi la Serikali liendelee." alisema Mhe. Sweda.
Mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana, na wenye ulemavu ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuimarisha ushiriki wa makundi hayo katika shughuli za kiuchumi, ikiwa ni hatua muhimu ya kupunguza umasikini na kuongeza fursa za ajira nchini.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe