Kwa kipindi Cha miaka mitatu Wilaya ya Njombe imepata hasara ya Shilingi Bilioni 316 kwa kuunguliwa na hekta 16,980 ambapo jumla ya mioto 51 iliripotiwa katika Halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Mji Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Akiwasilisha taarifa ya ripoti ya mioto katika Wilaya ya Njombe Mhifadhi wa Misitu Mwandamizi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS Wilaya ya Njombe Audatus Kashamakula amesema kuwa hasara hiyo ni kubwa na ambayo imerudiasha Maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na Taifa nyuma na hivyo jamii inapaswa ielimike na kuachana na tabia hii inayoingizia Mkoa hasara kubwa.
"Zipo sababu mbalimbali ambazo zimekua zikipelekea vyanzo vya moto.Zipo sababu za kichuki, migogoro lakini pia kumekuwa na tabia ya kuandaa mashamba kienyeji na bila kuchukua tahadhari stahiki wakati wa maandalizi ya mashamba na hivyo kupelekea moto kutoroka, kusambaa na kuingia katika mashamba ya majirani"Alisema Audatus
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa onyo kwa Wananchi ambao wanasababisha mioto kichaa na kuwataka Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria na kanuni za mazingira ikiwa ni pamoja na kuwasajili kwenye kila Kijiji Wananchi wote wanaojishughulisha na Kilimo.
Aliendelea kusema kuwa hayupo tayari kuona Wawekezaji katika Sekta ya miti wakikimbia kuwekeza Mkoani Njombe kwa hofu ya kuunguliwa mashamba yao.Halmashauri ya Mji Njombe kwa kipindi Cha Mwezi Julai -Oktoba mwaka 2022/2023 imepata hasara ya Bilioni 1.9 ambapo jumla ya hekta 105 zimeungua kwa moto na mwaka 2021/2022 hekta 7356 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 137 zimeteketea kwa moto
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe