Baraza kuu la Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Mji Njombe Februari 26,2024 limekaa kujadili rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 ambapo limepitisha bajeti ya shilingi bilioni 46.2.
Kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Halmashauri ya Mji Njombe inakisia kukusanya jumla ya shilingi 46,264,751,865.46 ambapo mapato ya ndani ni shillingi 9, 404,602, 286.5 ruzuku ya mishahara na matumizi mengineyo shillingi 27 ,800,365,000 ruzuku maendeleo shillingi 4,857,670,000 na ruzuku ya maendeleo kutoka kwa wahisani shillingi 4, 202,114,000.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete ameeleza vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni kutatua changamoto za wananchi kwa kuboresha miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya, elimu ya awali na msingi pamoja na miundombinu mingine ikiwemo barabara sambamba na kusimamia kikamilifu afua za lishe ili kutokomeza udumavu ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe.
Aidha Mhe Erasto Mpete kwa niaba ya Baraza Kuu la Madiwani amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuleta fedha mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji na barabara.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe