Mwili wa aliyekuwa mwalimu wa shule msingi Sinai iliyopo kata ya Mji Mwema mwalimu Agnetha Mlowe, Aprili 22,2024 umepumzishwa kwenye makao ya milele, kijiji cha Igagala Wilayani Wanging'ombe.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Shida Kiaramba ambaye ni Mkuu wa Idara ya elimu ya msingi na awali Halmashauri ya Mji Njombe, ametoa salamu za pole kwa wafiwa wote hasa ndugu wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao mwalimu Agnetha Mlowe
Bi. Shida alieleza wasifu wa marehemu ulioleta matokeo chanya wakati wote wa utumishi wake kama mwalimu.
" Katika utumishi wa umma wa mwalimu Agnetha Mlowe amesaidia sana kuinua taaluma katika shule ya Msingi Sinai" alisema Bi. Shida Kiaramba.
Aidha alitumia fursa hiyo kuhimiza uwajibikaji kwa waalimu wengine.
"Mnapoona umati huu ni kwasababu, mwalimu Agnetha Mlowe katika utumishi wake alikuwa mchapakazi sana na alikuwa mfano wa kuigwa kwa walimu wengine.Niwaombe waalimu wengine muige mfano wake."
Tukio la kumpumzisha lilitanguliwa na Misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa katoliki Kigango cha ya Nazareth parokia ya Njombe Mjini.
Raha ya milele umpe Ee Bwana ,na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa Amani "
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe.Amina.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe