Halmashauri ya Mji Njombe imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wagawa dawa ngazi ya jamii (CDD) ili waweze kwenda kutoa huduma kwa ufanisi .
Mafunzo hayo yametolewa Februari 21,2024 na Mfamasia wa Halmashauri ya Mji Njombe Beni Ngogo akishirikiana na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ambapo aliwaomba wagawa dawa hao kwenda kugawa dawa za magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele (usubi, matende na mbusha, trakoma, kichocho na minyoo ya tumbo) kwa kuzingatia taratibu na miongozo ambayo imewekwa na kwa kufuata taaluma.
Katika mafunzo hayo watoa huduma vituoni waliagizwa kwenda kuwajengea uwezo wagawa dawa ngazi ya jamii (CDD) watakaoshirikiana nao kwenye zoezi hilo kwa kuwaeleza majukumu yao katika zoezi ya ugawaji wa dawa.
Zoezi hilo la kugawa dawa kinga hizo linatarajia kuanza siku ya Jumapili Tarehe 25 Februari 2024 kwa watu wote wenye umri wa kuanzia miaka mitano nakuendelea isipokuwa wajawazito na wagonjwa mahututi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe