Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt. Jabir Juma, amewatoa hofu wazazi na walezi juu ya chanjo ya surua na Rubella iliyoanza kutolewa Februari 15,2024.
Dkt Jabir katika Uzinduzi wa kampeni hiyo kimkoa, amesema chanjo hiyo ni salama na itasaidia kuwakinga watoto na magonjwa ya mlipuko ya surua na Rubella hivyo ni vyema kila mzazi akazingatia Mtoto wake kupatiwa chanjo hiyo.
Kampeni ya chanjo ya surua na rubella inafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 15 hadi 18 Februari 2024.
Katika Halmashauri ya Mji Njombe chanjo inatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, shuleni na maeneo mengine ya mikusanyiko.
Lengo la ni kuchanja watoto 16,164 wenye umri chini ya miaka 5 na wasiopungua miezi 9 kwenye kata zote za Halmashauri ya Mji Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe