Jumla ya Watahiniwa 4613 wakiwemo Wasichna 2275 na Wavulana 2338 wanataraji kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la Saba kutoka Halmashauri ya Mji NjombeKaimu Afisa Elimu Halmashauri ya Mji Njombe Festo Salingwa amesema kuwa Watahiniwa hawa pia ni zao la kwanza la Mpango wa Serikali wa Elimu bila malipo ambapo ulianza mwaka 2015 ambapo kwa kipindi chote hicho Wanafunzi wapatao elfu Moja wameongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita.
Akizungumza na Wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani katika Shule mbalimbali Mjini Njombe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick amewataka Wanafunzi hao kufahamu ya kuwa safari yao ya mafanikio inakwenda kuanza na kuandika hivyo hawana budi kuhakikisha wanafanya vyema mitihani hiyo.
"Katika kipindi chote Cha miaka Saba Waalimu wameweza kuwafundisha ipasavyo.Hivyo ni muda wenu kutumia siku mbili Yale yote mliyofundishwa kuweza kuyajibu kwenye mitihani.Ninaamini wote mtafaulu na kwenda kidato Cha kwanza.Mheshimiwa Rais ametoa nafasi kwa Wanafunzi kuanzia kidato Cha kwanza mpaka Cha sita kusoma bila gharama zozote.Hivyo ni fursa kwetu tuitumie nafasi hii kufanya vizuri"Alisema
Aliendelea kusema "Safari ya mafanikio yetu inakwenda kuanza kesho na tukumbuke kuwa maisha ya Wazazi wako sio maisha yako.Maisha yako sio ya Wazazi wako wewe unakwenda kuanza maisha yako bora zaidi na yenye mafanikio bila kujalisha hali ya kipato Cha mzazi"Alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Watahiniwa hao kutoka katika Shule ya Msingi Viziwi,Ruhuji,Kambarage na Utalingolo wamemshukuru Mkurugenzi kwa kuzungumza nao masaa machache kabla ya mtihani na wameahidi kupata ufaulu mzuri kwenye matokeo hayo ili waweze kupata nafasi ya kuingia kidato Cha kwanza kwenda mbele zaidi.Rai imetolewa kwa wazazi kuwapunguzia mzigo wa Majukumu ya majumbani Watahiniwa hao kwa kipindi hiki Cha mitihani ili wautumie muda huo kusoma na kujipanga kwa mitihani inayofuata.
Baadhi ya Shule zilizopata nafasi ya kutembelewa na kupewa salamu na heri ya mitihani kwa niaba ya Shule nyingine ni Mjimwema,Viziwi,Ruhuji,Kibena,Kambarage na Utalingolo Shule ya Msingi
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe