Uongozi wa soko Kuu Njombe kwa kushirikiana na Idara Maendeleo Jamii Halmashauri ya Mji Njombe kitengo cha ukatili wa kijinsia imeunda dawati la kutoa elimu ya ukatili na kupinga ukatili wa kijinsia katika Soko Kuu Njombe ilikuweza kusaidia kuripoti vitendo vya ukatili vinavyo tokea katika eneo hilo.
Akizungumza Julai 11,2024 na wafanya biashara wa soko kuu Njombe baada yakuunda timu ya viongozi wakusimamia dawati hilo ,Zawadi Tweve Katibu wa Soko amesema timu hiyo itashirikiana kuandaa mpango wa kuhakikisha vitendo vya ukatili vinavyotokea katika soko hilo vinaripotiwa kwenye mamlaka husika na kufanyiwa kazi kwa wakati ili kuondoa kabisa ukatili kwa makundi mbalimbali katika jamii.
Kwa Upande wake Ahaz Kinyamagoha Afisa maendeleo ya jamii, Halmashauri ya Mji Njombe amesema pamoja na majukumu mengine timu hiyo itakuwa ikitoa elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na kushirikiana na uongozi wa eneo husika kuhakikisha huduma ya rufaa kwa walio fanyiwa vitendo vya ukatili inayolewa kwa wakati.
Timu hiyo inaundwa na wajumbe kumi (10) wanne(4) kutoka kwa wafanyabiashara wa soko kuu Njombe na wajumbe (6) kutoka Ofisi ya Meneja soko kuu pamoja na Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Njombe Mjini.
Maeneo yote ya masoko,vituo vya mabasi bajaji na bodajoda katika Halmashauri ya Mji yatafikiwa na wataalam kwa ajili ya kuunda dawati la kutoa elimu na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe