Ikiwa ni katika muendelezo wa ziara ya kikazi ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe yenye lengo la kutembelea Wananchi ,Kujifunza mazingira changamoto,kuzipatia ufumbuzi na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo hayo ,Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata ya Matola wamfurahisha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe kutokana na ubora wa miradi na thamani halisi ya fedha.
Akizungumza mara ya kutembelea na kukagua nyaraka za mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kitulila ambapo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 26 ikiwa katika hatua za mwisho za ukamilishaji na ujenzi wa nyumba ya mganga ambapo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 17 kufikia hatua ya lenta,Mkuu wa Wilaya amesema kuwa miradi hiyo imejengwa kwa ubora na thamani ya fedha iliyotumika inaonekana.
“Kuna maeneo mengine unapita unashindwa kuelewa fedha zimefanya kazi gani. Niwapongeze sana Kata ya Matola kwa kazi kubwa mliyofanya.nyaraka zote zipo.Nitoe wito kwa watendaji kufuata mfano wa mwalimu huyu.Mchanganuo wa fedha upon a unaelezeka kwa kweli ni wapongeze maana mmenipa matumaini.Alisema Mkuu wa Wilaya.”
Edwin Mwanzinga ni Diwani wa Kata ya Matola ambaye amesema kuwa siri kubwa ya mafanikio katika Kata hiyo yaliyopelekea kufanikisha ufanisi wa miradi hiyo ni kuwa kumekuwa na ushirikiano mkubwa baina ya Wataalamu na Viongozi katika Kata hiyo ambapo ushirikaino huo umepelekea kuibua miradi kuanzia ngazi ya chini na taarifa zote za matumizi ya fedha zinajulishwa kwa kila ngazi ili kuwa na uelewa wa pamoja. Wote tunazungumza lugha moja”Alisema Mwanzinga
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Njombe ameagiza Wahandisi kuendelea kusimamia ujenzi wa miradi na kuwa na makisio sahihi kwa ufanisi ili fedha zilizokusudiwa kupelekwa kwenye miradi ziweze kumaliza miradi hiyo na kuepuka miradi kuongezewa fedha mara kwa mara au wananchi kuchangishwa michango mara kwa mara jambo linalokatisha tamaa Wananchi na pia kupelekea miradi kutokamilika kwa wakati.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe