Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mheshimiwa Kissa Gwakisa akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe na Viongozi mbalimbali kwenye Ziara ya kukagua mwenendo wa zoezi la Sensa Katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Njombe.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Yakobi, Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi ambao bado hawajafikiwa na Makarani wa Sensa kuendelea kuwa wavumilivu kwani zoezi la sensa litafanyika kwa muda wa siku Saba kuanzia tarehe rejea ya sensa 23 Agosti 2022 na hivyo kuendelea kuwa na subira.
"Kitu ambacho kimenifurahisha ni kuwa watu wameendelea kubaki nyumbani kusubiria Makarani.Lakini nipongeze kwani mpaka sasa zoezi linaenda vizuri kwani wameweza kuandikisha robo tatu ya watu wa eneo hili."Alisema Kissa.
Aliendelea kusema, " Niwaombe Wananchi ambao bado hawajafikiwa kuwa watulivu na Wenye subira kwani wote tutafikiwa na kuhesabiwa"Alisema.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji na Mabalozi kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi kuwa zoezi la Sensa linaendelea kwa muda wa siku Saba ili kuwajengea uwezo zaidi.
Nao baadhi ya Wananchi katika Kata ya Yakobi ambao walipata bahati ya kutembelewa na Viongozi hao wamemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya na Mkurugenzi kufika na kujionea zoezi hilo ambapo wameahidi kutoa Ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha kwa kishindo zoezi hilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe