Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mheshimiwa Kissa Gwakisa Kasongwa, ametoa wito kwa wazazi wenye watoto waliotimiza miaka 18 ambao ni wanafunzi kuruhusiwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Tarehe 27 Novemba 2024.
"Hapa tunawaona wanafunzi ,wanasifa za kujiandikisha wana miaka 18,niombe Wazazi wenye watoto waliotimiza umri wa miaka 18, muwaruhusu kuja kujiandikisha ili waweze kupiga kura" alisema Mhe. Kasongwa Akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Hagafilo waliofika kujiandikisha kwenye kituo kilichopo ofisi ya Mtaa wa Lunyanywi,ambapo umefanyika uzinduzi wa uandikishaji Kimkoa.
Aidha, Mhe. Kasongwa ametoa wito kwa viongozi mbalimbali na wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye maeneo yao, akiwapongeza wale wanaoendelea kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato mzima uchaguzi.
Mhe.Kissa,Mkuu wa Wilaya ya Njombe amejiandikisha katika kituo kilichopo kwenye mtaa wake wa Mgendela Kata ya Njombe Mjini,Halmashauri ya Mji Njombe.
Uandikishaji wa wapiga kura utafanyika kwa siku 10 na vituo vya kuandikisha wapiga kura vitafunguliwa saa 2Asubuhi na kufungwa saa 12 Jioni.
Kajiandikishe
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi Jitokeze Kushiriki Uchaguzi ".
@ortamisemi
@kissagwakisakasongwa
@ms_mhaiki
@njombe_rs
@anthony_mtaka
@mohamed_mchengerwa
@
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe