• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

DC Njombe abisha hodi Halmashauri ya Mji Njombe.Ateta na Watumishi na kuwataka kuchapa kazi

Tarehe iliyowekwa: July 9th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano na kutekeleza matarajio ambayo Serikali imeweka kwa Wananchi wake kwa kuzingatia  sheria, kanuni na taratibu ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuepusha migogoro katika kufanya maamuzi na kutekeleza kazi za kufikisha maendeleo kwa Wananchi.

Mhe. Kissa amesema kuwa katika kusukuma gurudumu la Maendeleo na kuifanya Njombe kuwa mbele usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ni jambo ambalo anatarajia kulianza  na amepanga kufanya ziara za kushtukiza na ziara rasmi ili kujionea utendaji halisi uliopo katika Sekta ya Afya na Elimu na amewataka Watumishi wa Sekta hizo kujiandaa na kurekebisha kasoro ambazo pengine zinaweza kuleta kero kwa Wananchi kwenye maeneo hayo. Aidha ametaka katika kila miradi uwepo wa nyaraka zote muhimu.

Akipokea taarifa fupi ya utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kwa mwaka 2020/2021 katika Halmashauri taarifa iliyowasilishwa na Mchumi wa Halmashauri Emma Lunojo Mhe. Kissa ameipongeza Halmashauri kwa kazi nzuri iliyofanyika.

“Taarifa hii inaonesha picha halisi ya uchapakazi, uzalendo na ari ya kuleta matukio makubwa kwa Nchi ya Tanzania. Niwapongeze kwa Kazi kubwa ambayo mmeifanya. Tufanye kazi kwa ubunifu. Sisi tumepata bahati ya kufanya kazi kwa niaba ya Watanzania wengine wote. Wote wangeweza kupewa nafasi Ila tumepewa dhamana kwa ajili ya wengine” Alisema Mkuu wa Wilaya

Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa ni kuhakisha kuwa Watumishi wanawahudumia Wananchi kwa Wakati na kutumia busara na hekima katika kuwaelekeza Wananchi wanaofika kupata huduma na kuacha tabia ya kuwashambulia Wananchi kwa maneno yasiyofaa.

Akitoa salamu za Shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt. Yesaya Mwasubila amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuteuliwa na hatua aliyoichukua ya kuja kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri hiyo na amesema kuwa yale yote ambayo ameyaelekeza yatakwenda kutekelezwa na kuahidi ushirikiano mkubwa katika kazi.

Mara baada ya kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongo leo amezungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe na anataraji kuanza ziara ya kikazi katika Wilaya ya Njombe kuanzia Jumanne ya tarehe 13 Julai 2021 kwenye kila Kijiji, Mtaa na Kata.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. June 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI NJOMBE TC AAGANA NA TIMU ITAKAYOCHEZA SHIMISEMITA.

    August 12, 2025
  • LISHE NA AKIBA YA MAZAO YAHIMIZWA NANENANE.

    August 08, 2025
  • KHERI YA SIKUKUU YA WAKULIMA 88 2025.

    August 08, 2025
  • ELIMU YA UNYONYESHAJI YATOLEWA KWA WAKAZI WA LWANGU

    August 05, 2025
  • Angalia zote

Video

ZIFAHAMU FAIDA ZA HERENI YA KIELEKTRONIKI KWA NG'OMBE.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe