Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, wakiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe, Bi. Agatha Mhaiki, tarehe 1 Agosti 2025, wametembelea banda la Halmashauri ya Mji wa Njombe katika maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Viongozi hao wamejionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe, ambao wamewezeshwa kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri (asilimia 4 kwa wanawake, asilimia 4 kwa vijana na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu).
Maonesho ya wakulima (Nanenane) ni fursa kwa wananchi kujifunza, kuonesha bidhaa, na kubadilishana uzoefu katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na ujasiriamali.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe