Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe.Juma Sweda ,Julai 24,2025 amempokea rasmi mkandarasi kampuni ya China National Aero Technology International Engineering Corporation,atakatekeleza ujenzi wa barabara za lami chini ya Mradi wa TACTICS awamu ya pili katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Serikali kupitia mradi wa TACTICS awamu ya pili itatumia Shilingi Bilioni 20.7 kujenga barabara za lami zenye urefu wa KM 8.4 katika Halmashauri ya Mji Njombe. Mkandarasi amekabidhiwa rasmi maeneo ya ujenzi Julai 23, 2025 kuanza kazi, ikiwemo ujenzi wa ofisi ya mradi, madaraja na taa za barabarani.
Barabara zitakazojengwa ni barabara ya :
• NBC-Kibena (KM 2.84)
• Chaugingi–Nzengerendete (KM 1.57)
• Nzengerendete–Masaki (KM 1.43)
• Magereza–Matalawe (KM 1.12)
• Mpechi–Melinze (KM 1.3)
Mhe.Sweda ametoa wito kwa mkandarasi huyo kuzingatia ubora, muda na thamani ya fedha, huku akisisitiza ushirikiano kati ya mkandarasi, wataalam wa TARURA na Halmashauri na wananchi.
Muda wa utekelezaji wa mradi huo ni wa miezi 15 hivyo utakamilika Oktoba 2026 na unatarajiwa kutoa ajira na kuinua uchumi wa wakazi wa Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe