Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mheshimiwa Juma Sweda, Septemba 22 ametembelea eneo la stendi ya zamani mjini Njombe na kujionea namna wananchi wanavyopatiwa huduma mbalimbali zinazotolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Huduma hizo ni pamoja na uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, huduma za kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na ufugaji nyuki na afya.
Katika ziara hiyo, Mhe. Sweda alieleza kuridhishwa na mwitikio wa wananchi kujitokeza kupata huduma hizo muhimu na kuwataka waendelee kutumia fursa hiyo ili kuboresha maisha yao.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe