Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick,Mei 22,2024 amefungua mafunzo kuhusu Bodi ya Bima ya Amana (DIB) yenye lengo kutoa elimu kuhusu Bodi ya Bima ya Amana, majukumu yake na masuala ya ufilisi wa iliyokuwa Benki ya wananchi ya Njombe (NJOCOBA).
Bi. Kuruthum amewataka washiriki wote kutumia mafunzo hayo kutoa michango yao ili Bodi ya Bima ya Amana iendelee kutekeleza vyema majukumu yake nakuendelea kuwa na tija kwa jamii na sekta ya fedha kwa ujumla.
Pamoja na mafunzo hayo taarifa ya ufilisi wa iliyokuwa Njombe Community Bank(NJOCOBA) iliyofungwa mwaka 2018 na kuwekwa chini ya ufilisi wa Bodi ya Bima ya Amana itatolewa ambapo zitatolewa takwimu za waliokwisha kuchukua amana zenye kinga ya bima ya amana ,stahiki za ufilisi pamoja na majina ya ambao bado hawajachukua stahiki zao.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa watendaji wa vijiji na mitaa,maafisa ushirika,maafisa maendeleo ya Jamii , pamoja na maafisa habari kutoka Halmashauri tatu za Wilaya ya Njombe ambazo ni Halmashauri ya Mji Njombe,Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji Makambako.
Mfumo wa Bima ya Amana ni utaratibu unaokusudiwa kuwakinga wenye amana dhidi ya kupotea kwa amana zao katika tukio la kushindwa au kufilisika kwa Benki au taasisi ya fedha.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe