• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

EFM WAFANYA TAMASHA NJOMBE KUHAMASISHA CHANJO

Tarehe iliyowekwa: August 14th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Njombe  Kissa Kasongwa amesema wapo kwenye jitihada za kuongeza idadi ya watu wanaochanja chanjo ya UVIKO 19 kwenye wilaya hiyo, na ndiyo maana wanafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandaa matamasha. Aliyasema hayo Agosti 13, 2022 kwenye tamasha la Mziki Mnene lililoratibiwa na Efm Redio kutoka Dar es Salaam na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kufadhiliwa na Epic/ FHI 360 kwa ajili kuhamasisha wananchi wachanje chanjo ya UVIKO 19, ambalo tamasha hilo lilifanyika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

"Tupo kwenye jitihada za kuongeza idadi ya wananchi wanaochanja chanjo ya UVIKO 19. Nia yetu ni kuona asilimia 70 ya wananchi wa Wilaya ya Njombe wanakuwa wamechanja. Wataalamu wanasema, kama asilimia 70 wataweza kuchanja, itakuwa ni kinga kwa wengine" alisema Kasongwa wakati anazungumza na wanahabari pembeni ya tamasha hilo.

Akizungumza na wananchi kwenye tamasha hilo, Kasongwa aliwaasa wananchi kujitokeza kwa hiari yao na kuchanja chanjo ya UVIKO 19 ili waendelee kuwa salama, na kuendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani.

'Ujanja ni kuchanja. Kuchanja sio suala la mzaha. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametutaka tuchanje kwa hiari yetu ili tuwe salama. Hata Shirika la Afya Duniani (WHO) linatutaka tuchanje. Tukichanja tutaushi, ila tukiacha kuchanja tutakufa. Tuhakikishe tunachanja na kuepukana na ugonjwa huu wa hatari" alisema Kasongwa akiwa amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka kwenye tamasha hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya zoezi hilo la uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19 kukamilika, Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Mji Njombe Simon Ngassa, alisema watu waliojitokeza kuchanja kwenye tamasha hilo ni 4,563, ambapo wanaume ni 1,954 na wanawake 2,609.

"Lengo ni kuchanja watu 98,396, ambao Ni asilimia 70 ya watu wenye umri wa miaka zaidi ya 18.. Tulianza kuchanja Agosti 3, 2021, na hadi Agosti 13, 2022 tumechanja jumla ya watu  92,422 sawa na asilimia  93.

"Dira yetu ni kufikia lengo la asilimia 100 ifikapo Septemba 30 mwaka huu 2022. Kwa kushirikiana na wadau wetu FHI360,  na wadau mbalimbali kwa pamoja na mikakati ya hamasa ya matamasha makubwa, na ushirikiano wa  DC (Kasongwa) na Mbunge (Deo Mwanyika- Njombe Mjini) katika ziara ya kijiji kwa kijiji kuhamasisha chanjo kwa wananchi" alisema Ngassa.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe