Elimu ya Amali ni elimu inayolenga kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa, ujuzi, umahiri na stadi za ujasiriamali ili wachangie kikamilifu katika maendeleo.
Kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023),elimu hii inaunganisha masomi ya nadharia na vitendo kwa lengo la kumeongezea mwanafunzi ujuzi wa kazi, kujiajiri na kuajirika.
Wanafunzi wanaosoma Shule za Sekondari za amali hupata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika sekta mbalimbali kama vile viwandani,kilimo mashambani,sekta ya uvuvi na huduma mbalimbali za kijamii.
Lengo kuu ni kuhakikisha wahitimu wanatoka na ujuzi halisi unaohitajika sokoni, sambamba na mabadiliko ya teknolojia.
Elimu ya Amali ni daraja la mafanikio kwa vijana wa Kitanzania kutoka kwenye utegemezi na kuingia kwenye uchumi wa uzalishaji.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe