Wananchi wa Mtaa wa Mgodechi uliopo kata ya Ramadhani Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa elimu ya juu ya kupanga ,kupima na kumilikisha ardhi.
Elimu hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa idara ya Ardhi Halmashauri ya Mji Njombe Amos Luhamba kwenye mkutano uliofanyika mtaani hapo Agosti 11,2023.
Kaimu Mkuu wa idara ya Ardhi Amos Luhamba amesema mtaa huo ni miongoni mwa mitaa yenye maeneo mengi ambayo bado hayajarasimishwa kwa mujibu wa sheria ya mipango miji hivyo wametangulia kutoa elimu ili wananchi waweze kutambua umuhimu wa kumili ardhi iliyo rasimishwa.
Akizungumza na wananchi wa mtaa huo diwani wa kata ya Ramadhani Mhe.Nickson Nganyange amewasisitiza wananchi wa eneo hilo kutoa ushirikiano ikiwemo kulipa ada ya upimaji kwa wataalamu wa ardhi watakaofanya zoezi hilo lakurasimisha maeneo yao.
Aidha amesema zoezi hilo litakapokamilika litaenda kupunguza malalamiko na maushauri ya migogoro ya ardhi kwenye baraza la kata.
Halmashauri ya mji njombe kupitia idara ya ardhi inaendelea na zoezi la urasimishaji wa ardhi mtaa kwa mtaa na zoezi ambalo tayari limekamilika kwa mitaa ya Kihesa ,Mgendela ,Kambarage,Ramadhani na linaendelea Uwemba ,kifanya ,Magoda ,Wikichi na Nundu.
Halmashauri ya Mji Njombe ikiwa inatekeleza mpango kabambe inasisitiza wananchi kushiriki kupanga ,kupima na kumiliki maeneo yao ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi ,kuwa na mji uliopangwa vizuri wenye huduma za jamii ,kuongeza usalama wa miliki,ardhi kutumika kama dhamna na kuongeza thamani ya ardhi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe