Halmashauriya Mji Njombe imeendelea kupiga hatua kufikia malengo ya kutokomeza udumavu Mkoani Njombe.
Akiwasilisha taarifa ya Tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe katika Halmashauri ya Mji Njombe Julai 17 ,2023 Afisalishe Fransisca Mosha amesema,katika kipindi cha miezi mitatu(April – June, 2023) wamefanikiwa kutengeneza mbadalawa chakula tiba(locally made therapeutic milk)kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye utapiamlo.Chakula tiba hicho kimefanya vizurina kitaenda kupunguza utegemezi kutoka bohari kuu ya dawa(MSD).
Afisa Lishe Fransisca amesema katika kupambana na changamoto ya udumavu kwa watoto mkoani njombe Halmashauri ya Mji Njombe wameendelea kutoa elimu ya matibabu ya utapiamlo na katika kipindi cha miezimitatu(3)wameweza kutoa elimu hiyo ya matibabu ya utapiamlo kwenye vituosita(6) vilivyopo Halmashauri ya mji Njombe na jumla ya watoto watano (5) waliokuwa na tatizo la utapiamlo mkali kutoka maeneo mbalimbali wametibiwa nakupona.
Kwaupande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dk Yesaya Mwasubila ametoa rai kwa akina mama wajawazito kuzingatia mahudhurio ya kliniki wakati wote wa ujauzito hasa kufanya hudhurio la kwanza mapema,pamoja na kutumia dawa za kuongeza damu zina zotolewa ili kuimarisha afya za watoto kabla ya kuzaliwa.
Dk Yesaya Mwasubila pia ametoa msisitizo kwa wataalamu wanao fanya kazi kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya ,kuhakikisha wana wapatia mama wajawazito elimu ya lishe pamoja na dawa zote wanazo hitajika kupatiwa kwa kila hudhurio la kliniki linalofanyika.
Akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Gwakisa ,Katibu TawalaWilaya ya Njombe Ndg.Agatha Mhaiki amesisitiza ushirikiano wakutoa taarifa sahihi kwa ngazi zote kuanziavijiji, kata mashuleni hadi mkoa ili kuwezesha kampeni ya kutokomeza udumavu mkoani njombe kufanikiwa.
Kwa suala la kushiriki na kufanya mikutano ya kuhamasisha kuhusu Lishe Bora ngazi ya kata Katibu Tawala wilaya ya njombe Agatha Mhaiki amewataka watendaji wote wa kata kutolegalega,kwa kuhakikisha mikutano hiyo inafanyika kwa utaratibu uliopangwa ili kufikia lengo kwa pamoja.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe