Wananchi wa Mtaa wa Idundilanga kata ya Njombe mjini halmashauri ya mji Njombe, wamepatiwa elimu ya lishe bora kwa watoto ili kuepukana na udumavu na utapiamlo ambao umekuwa changamoto Mkoni Njombe.
Akitoa elimu ya lishe katika mkutano wa afya na lishe mtaa wa idundilanga Afisa Lishe wa Halmashauri ya mji Njombe Damiana Danda amesema mapambano dhidi ya udumavu yaanzie pale mama anapopata ujauzito,kwa kuhakikisha anapata lishe bora kipindi chote cha ujauzito na kuzingatia lishe bora kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano(5).
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Idundilanga Dr Kenedy Elisha amewaomba wazazi kuwa karibu na wataalamu wa afya na lishe ili kupata ushauri pale wanapopata changamoto yoyote inayohusu lishe kwa watoto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Idundilanga Filoteus Ngilangwa amewataka wananchi hao kuzingatia elimu waliyoipata ili kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na afya njema
Mpaka sasa Elimu ya lishe imetolewa katika mitaa 4 kati ya 9 iliyopo kata ya Njombe Mjini
#njombebilaUdumavuinawezekana
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe