Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Njombe,Fransisca Mosha katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) iliyofanyika Mei 28,2024 kijiji cha Luponde ,amewaomba wanaume kuzingatia siku hiyo ya lishe ambayo huadhimishwa kila baada ya miezi 3,kwa kushiriki pamoja na wake zao kwa kuwa elimu lishe inayotolewa ni kwa ajili ya wazazi wote(Baba na Mama).
“Niwaombe wamama mliohudhuria leo ,ukifika nyumbani mweleze baba elimu uliyopatiwa ,na muwaambie kuwa siku ya afya na lishe si ya wanawake peke yao ,wanatakiwa kushiriki ili muweze kusaidiana kwenye suala zima la lishe kwa watoto”.Alisema Fransisca Mosha ,Afisa lishe Njombe Mji.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe