• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Halmashauri ya Mji Njombe
Halmashauri ya Mji Njombe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Halmashauri ya Mji Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Elimu ya Mpango wa Urasimishaji ya MKURABITA itolewe kwa Wananchi

Tarehe iliyowekwa: January 25th, 2020

Elimu ya manufaa yatokanayo na  mpango wa Urasimishaji inayoendeshwa na MKURABITA Kwenye Halmashauri zinazonufaika na mpango huo bado ni changamoto kubwa inaowakabili Wananchi kwani wengi wao bado hawana uelewa wa kutosha juu manufaa ya  Urasimishaji.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa (Mb) kwa Watendaji wa Halmashauri kwenye ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Njombe iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya MKURABITA katika Halmashauri hiyo na kuwataka Watendaji kwenye Halmashauri zinazonufaika kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa ya Urasimishaji  Ardhi na Biashara zao.

Dkt.  Mwanjelwa amesema kuwa licha ya kuwa Halmashauri imefanya vizuri katika kutekeleza mpango huo bado elimu iliyotolewa haijitoshelezi jambo ambalo lisipotiliwa mkazo linaweza kusababisha migogoro.

“MKURABITA ni ya Wananchi, Urasimishaji ni kwa ajili ya Wananchi. Waelezeni  bayana  Wajibikeni kwa Wananchi kwa kutoa huduma ipasavyo.”Alisema Mary Mwanjelwa.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ametoa maelekezo kwa Wasimamizi   wa Urasimishaji kuhakikisha kuwa mashamba ya miti na parachichi yanapimwa kwa kadri wananchi walivyoomba ili Wananchi waweze kupata hati za mashamba yao.

Wakielezea kwa Nyakati tofauti tofauti baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji “Chambinga Workshop, Nahala na Mama Seki” wamesema kuwa manufaa waliyoyapata  ni pamoja na kupata mikopo katika Taasisi mbalimbali za kifedha jambo ambalo limewasaidia kuendeleza biashara zao na kuboresha hali za maisha katika familia zao.

Halmashauri ya Mji Njombe imefanikiwa Kurasimisha viwanja na nyumba 8,782 na jumla ya wafanyabiashara 129 waliweza kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi 899,499,488/= kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha yote ikiwa ni manufaa yaliyotokana na zoezi la Urasimishaji.










Matangazo

  • KUITWA KAZINI NA MAFUNZO TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 21, 2025
  • TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 19, 2025
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTAKA AONGOZA MAOMBI YA AMANI KWA TAIFA.

    November 07, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO NJOMBE MJINI AFUNGUA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA .

    October 26, 2025
  • MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA 366 WAAPISHWA NA KUPATIWA MAFUNZO JIMBO LA NJOMBE MJINI.

    October 25, 2025
  • KUBWA KULIKO KUWAHI KUTOKEA NJOMBE MJINI

    October 20, 2025
  • Angalia zote

Video

TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe