Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Njombe Agosti 26,2024 limefanya mafunzo ya tahadhari kwa watumishi wa Makao Makuu na vituo vya afya katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha watumishi hao kujua mbinu za kujiokoa na kuokoa mali wakati wa dharura haswa katika majanga ya moto.
Mafunzo hayo pia yalihusisha utoaji wa elimu ya namna ya kutumia vifaa vya kuzimia moto, ikiwemo vizimia moto na mifumo ya tahadhari, ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.
Pamoja na mafunzo hayo washiriki wamehimizwa kutumia namba ya dharura 114 kwa usahihi ili kufanikisha uokoaji wa watu na mali zao katika majanga.
Hii ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Zimamoto kutoa elimu ili kuongeza uelewa na uwezo wa jamii kukabiliana na majanga.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe