Wakulima wa zao la Parachichi Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa mafunzo ya namna ya utunzaji Wa maua na matunda ya parachichi.
Elimu Hiyo imetolewa kwa wakulima Juni 09,2023 na Idara ya kilimo, mifugo na uvuvi kwakushirikiana na Chama Cha Kijamii cha Wadau Wa Parachichi Tanzania (ASTA)ili kuwawezesha wakulima Wa zao la parachichi kupata tija kwa kuhudumia mashamba Yao kitaalamu.
Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthumu Sadick akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Amewapongeza wakulima hao,wengi wao wakiwa ni vijana huku akiwatia moyo kuendelea na kilimo cha zao la parachichi
Amesema Kuna fursa nyingi Sana kwenye kilimo hususani cha parachichi kwa mkoa wa Njombe akiwasihi vijana kutokata tamaa na kufikiria kuwa na mashamba yao binafsi ili wanufaike moja kwa moja na kilimo hicho.
"Ninafurahishwa Sana kuona vijana wengi, niwatie moyo msikate tamaa fanyeni jitahada hata kama mnatumika kwenye mashamba ya wengine muweze Kuwa na mashamba yenu"
Aidha amewasihi washiriki wote kuzingatia mafunzo hayo katika kuhudumia mashamba yao ili waweze kupata mazao bora ambayo yataleta ushindani sokoni na kwamba hivi Sasa mpango serikali nikuwataka wawekezaji kununua moja kwa moja kutoka kwa mkulima ili anufaike moja kwa moja.
Kwa upande wake Mtaalamu na mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Parachichi Tanzania Rebecca Hepelwa amesema wameamua kutoa elimu kwa wakulima juu ya utunzaji Wa maua na matunda kwani hatua ya maua ndiyo hatua muhimu kwenye zao la parachichi itakayomsaidia mkulima kupata tija kwenye kilimo cha parachichi.
Wakulima Hao pia wameelimishwa dawa sahihi za kutumiwa na wakati wakuzitumia huku akitoa angalizo kwa wakulima kuotumia dawa zakuulia wadudu kiholela wakati wa maua kwani wadudu wengi kipindi hicho wanakuwa wanafanya shughuli ya uchavushaji.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji Njombe yaliwajumuisha wamiliki, wakulima na wasimamizi wa mashamba ya parachichi na yalihitimishwa kwa washiriki hao Kujifunza kwa vitendo kwenye shamba la mfano lilipo kwenye viwanja vya Halmashauri ya Mji Njombe
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe