Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini amewaomba wafanyabiashara kuendelea kuiamini Serikali kwakuwa ni sikivu na inaendelea kusikia na kutatua kero mbalimbali za wafanyabishara.
Ameyasema hayo Mbunge Deo Mwanyika Januari 3 ,2024 katika Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe uliofanyika mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ndani ya Mji wa Njombe, kusikiliza nakutatua kero wanazokutana nazo kwenye maeneo yao ya biashara.
Mb. Deo Mwanyina amewaomba wafanyabiasha hao kuendelea kuiamini Seriakli ya awamu ya sita kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanyika kuhakikisha wafanyabiashara wanakuwa huru katika utekelezaji wa shughuli za kujipatia kipato.
Aidha Mhe. Mwanyika amesema kwa miaka 3 Halmashauri ya Mji wa Njombe kupifia mtandao wa barabara , Maji imepiga hatua kubwa kwani zaidi ya bilioni 54 zimetekeleza miradi mbalimbali ya maji na miradi mingine ikiendelea kutekelezwa huku miundombinu ya barabara ikizidi kuboresha
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Thadei Luoga amewaomba wafanyabiashara kuendela kufuata taratibu za nchi, akisisitiza wafanyabiashara kwenye maeneo yasiyo rasmi kuondoka katika maeneo hayo ili kuboresha mazingira ya Mji wa Njombe ambao ni kioo cha Mkoa.
Diwani wa kata ya Njombe Mjini Alatanga Nyagawa ameishukuru serikali ,Mbunge watalamu wote wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa kuendelea kushirikiana kutekeleza shughuli za maendeleo katika kata ya Njombe Mjini .
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe