Wananchi wote wanaodiwa kodi ya pango la ardhi wametakiwa kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ndani ya siku 30 zilizotangazwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Jerry Silaa ili kuepuka adhabu.
Rai hiyo imetolewa Mei 17,2024 na Kaimu Mkuu wa idara ya Ardhi Halmashauri ya Mji Njombe Emmanuel Luhamba wakati akitoa elimu kwa umma kuhusu agizo hilo katika kituo cha Redio Uplands FM kilichopo Mjini Njombe.
“Niwaombe wananchi wote wa Halmashauri ya mji Njombe kwa wale ambao hawajalipa walipe katika kipindi hiki cha msamaha, baada ya siku hizo sheria kali itachuliwa kwa wale ambao hawatatekeleza kwa kwa mujibu wa fungu la 50 la sheria ya Ardhi (sura ya 133)” alisema Emmanuel Luhamba Kaimu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Mji Njombe.
Kituo cha kutole huduma kinapatikana ofisi ya Meneja soko kuu Njombe kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Mei 10,2024 wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi iliwajulisha wananchi wote kuwa, Wanao wajibu wa kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka kwa mujibu wa fungu la 33(1) la sheria ya Ardhi sura ya 113.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe