Halmashauri ya Mji Njombe imefanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Baraza la Waheshimiwa Madiwani limempigia kura 15 za NDIO kati ya kura 15 Mheshimiwa Erasto B. Mpete Diwani wa Kata ya Utalingolo na kumpitisha kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Awali akielezea mambo ambayo atakwenda kuyasimamia Mheshimiwa Mpete amesema kuwa Miongoni mwa mambo muhimu ni katika kufanikisha usimamiaji wa bajeti iliyoanza kutekelezwa kwa Mwaka 2022-2023 na kuhakikisha kuwa Halmashauri inakwenda kufanya vyema katika zoezi la usimamizi wa mapato ili iweze kuendelea kuongoza na kuwa Halmashauri bora na mfano Nchini.
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary amepongeza Mheshimiwa Mpete kwa hatua hiyo na amesema kuwa kwa kipindi chote ambacho Mheshimiwa Mpete alikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri Ushirikiano ulikuwepo na aliweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo jambo ambalo liliweza pia kurahisisha utendaji Kazi hata katika ngazi ya Mkoa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Sure Mwasanguti amewataka Madiwani hao kuimarisha Umoja na Mshikamano na kuvunja makundi yote yaliyokuwepo kabla ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja ili kuweza kufikia Maendeleo lakini pia kuhakikisha kuwa Wananchi wote wanahudumiwa sawa na Maendeleo yanawafikia Wananchi wote bila ya kuwa na mgawanyiko.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri umefanyika kutokana na kifo Cha aliyekuwa Mwenyekiti na Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Romanus Mayemba na hivyo kuziba pengo hilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe