Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia TASAF Halmashauri Njombe wametakiwa kutumia fedha wanazopata kwenye shughuli ndogondogo ambazo zitawaingizia kipato ili kujikwamua hali mbaya kiuchumi na kundokana na umaskini .
Wito huo umetolewa Mei 20 ,2024 na Gladness Sanga mwezeshaji wa TASAF kijiji cha Mfereke Kata ya Utalingolo Halmashauri ya Mji Njombe.
"Niwaombe fedha hizi zitumieni vizuri wekezeni kwenye miradi midogomidogo ya kilimo na ufugaji ili muinue uchumi wenu Alisema Gladness Sanga mwezeshaji wa TASAF Kijiji cha Mfereke.
Aidha mwezeshaji huyo amewaomba wanufaika hao kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia pale ambapo wanafanyiwa wakiwa katika maeneo yao ya makazi ili kuweza kukomesha vitendo vya ukatili kwenye jamii.
TASAF Halmashauri ya Mji Njombe inaendelea na zoezi la ugawaji fedha kwa walengwa 36, 010 kwenye kata na mitaa yote kwa dirisha la malipo ya Januari na Februari 2024.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe