• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

FIDIA MILIONI 144.8 MRADI WA MAJI NJOMBE YAKAMILIKA

Tarehe iliyowekwa: March 6th, 2024

Serikali ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji Machi 06,2024, imekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia ya shilingi milioni 144.8 kwa wananchi waliotoa maeneo yao yenye ukubwa wa jumla ya hekari 6.06 kwa ajili utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa miji 28, utakaotekelezwa katika Halmashauri ya Njombe kata ya Mjimwema ,mtaa wa Lunyanywi kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Hagafilo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi za malipo hayo Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Bi. Agatha Mhaiki ametoa shukrani dhati na pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha zoezi zima la fidia pamoja jitihada zinazofanyika chini ya Wizara ya Maji na dhamira yake ya kumtua mama ndoo kichwani  kwa kumaliza kabisa tatizo la maji nchini.

Aidha amewataka wananchi hao  kutumia vizuri fedha waliyopatiwa kufanya maendeleo na kutafuta maeneo mengine ya makazi badala yakuzitumia kwenye mambo ya anasa.


Kwa upande wake diwani wa Kata ya Mji Mwema Mhe. Nestory Mahenge amesema uongozi wa kata upo tayari na kwa kushirikina na wananchi watatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa kipindi chote cha utekelezaji wa miradi huo ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Mradi wa maji wa miji 28 Mjini Njombe  utagharimu dola za kimarekani milioni 15 ambazo zitajumuisha; ujenzi wa tegeo la maji,ujenzi wa njia kuu ya maji yenye urefu wa kilomita 2.5,ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji,ujenzi wa tenki la maji  lenye ujazo wa lita milioni 1 pamoja na kilomita 40 za mabomba yakusambaza maji.


Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa  kwa kipindi cha miezi 30 na kukamilika kwa mradi huo kutawezesha upatikanaji wa maji ya uhakika katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe ikiwemo Lunyanywi,Mjimwema,Msete,Ngalanga,Stendi mpya ya mabasi,Wende na Hagafilo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe