Halmashauri ya Wilaya ya Hai yatembelea Halmashauri ya Mji Njombe kwa lengo la kujifunza kilimo cha parachichi na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumza Oktoba 02 ,2024 ulipo wasili ugeni huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Kuruthum Sadick ameishukuru na kuipongeza Halmashauri hiyo kwa kuona fursa mbalimbali za kilimo cha parachichi katiika halmashauri ya mji njombe ambapo wanachi wengi wamekuwa wakinufaika kupitia zao hilo
“Nimefurahi sana kuona mmekuja kututembelea halmashauri yetu ,naamini hamtatoka kama mlivo kuja na sisi pia tutajifunza vitu kutoka kwenu ambavyo vitasaidia halmashauri yetu kusonga mbele na kukua zaidi kiuchumi” Alisema Kuruthum Sadick Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Hai Mhe.. Edmund Rutaraka amesema kwa fursa za kilimo hasa cha parachichi ambazo wameweza kuziona zitaenda kuimarisha uchumi wa wananchi wa hai kutokana fursa ambazo wameziona zitakwenda Kunyanyua uchumi wa wawana wilaya hiyo hasa katika kilimo hicho ambacho kimekonga Nyoyo zao kwa namna wananch wa njombe wanavyo nufaika kwa maelfu ya fedha kupitia kilimo hicho
Halmashauri ya wilaya Hai imetembelea Shamba la Mkulima wa Prachichi Nemes Green Garden , Soko Kuu Njombe namna linavyo fanyakazi vizuri na Kiwanda cha kuchakata Parachichi kilichopo Hagafilo kata ya Njombe Mji.
Ziara ya Halmashari ya wilaya ya Hai na Njombe mji italeta mapinduzi makubwa katika uchumi wa wananchi wa halmashauri hizo kwani wataenda kuibua miradi mipya ambayo itakuwa na tija na yenye ufanisi mkubwa pamoja kuongeza diplomasia chanya ya halmashauri hizo..
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe