Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka Januari 17,2024 amefanya ziara katika shule ya Msingi Nazareth iliyopo Halmashauri ya Mji Njombe ambapo amepata fursa yakuzungumza na wanafunzi kuhusu taaluma sambamba na kufikisha ujumbe wa lishe kupambana na udumavu Njombe kwa jamii.
Mheshimiwa Mtaka amewataka waalimu wanaofundisha masomo ya sayansi shuleni kutilia mkazo kwenye somo lishe ili wanafunzi waweze kuwa na uelewa mkubwa kuhusu makundi ya vyakula,lishe bora pamoja na umuhimu wakupata mlo ulio kamili kila siku.
Aidha amewataka wazazi na walezi wa Mkoa wa Njombe kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule bila vikwazo vyovyote pamoja na kuzingatia lishe bora kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wajawazito na vijana wa rika balehe ili kupambana na udumavu Mkoani Njombe.
Sambamba na hilo amewaeleza wananafunzi kuwa ni muhimu kuwakumbusha wazazi na walezi wao kuwapatia mlo kamili kama ambavyo wanafundishwa kwa kuzingatia makundi yote ya chakula ambayo ni wanga,protini,jamii ya mikunde,mbogamboga ,matunda ,mafuta ,madini pamoja na kunywa maji yaliyo safi na salama.
Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Njombe upo kwenye kampeni maalumu ya kupambana na udumamavu inayohamasisha jamii umuhimu wa lishe bora kwa watoto.Kampeni hiyo inasema Lishe ya Mwanao ,Mafanikio yake na kauli mbiu ya kampeni hiyo inasema “Kujaza tumbo sio Lishe ,Jali Unacho Mlisha”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe