Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka amesisitiza elimu ya lishe kuwa ni agenda muhimu kwenye mikutano mbalimbali ya vyama vya siasa,kwenye nyumba za ibada na maeneo mengine yanawakusanya wananchi.
Amesema hayo Mhe Mtaka Januari 27,2024 kwenye kilele cha kampeni yakuongeza kasi ya kupunguza udumavu Mkoani Njombe kilichofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya zamani Njombe Mjini.
“Niwaombe viongozi wangu wa dini na wa kisiasa kwenye salamu zetu tuongeze na hii ya Lishe ya Mwanao Mafanikio Yake ,Kujaza tumbo Sio Lishe,Jali unachomlisha”Alisema Mhe.Mtaka.
Aidha amesisitiza kila familia kutathimini mlo wanaoupata nyumbani kila siku kama ni mlo kamili.
Mhe .Mtaka alieleza kuwa kampeni ya kuhamasisdha lishe bora imefanyika kwenye Halmashauri sita za Mkoa wa Njombe na kwa kipindi cha mwezi mmoja wamewafikia watu zaidi ya 1,500 sambamba na kufanya kliniki za wamama wajawazito na kinamama wanaoonyonyesha.
Wakati wa kampeni Wilayani mijadala ilifanyhika ikihusisha na makundi viongozi wa dini, makundi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wakiongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini pia makundi ya kinamama na baba lishe na kundi la vijana .
Pia mikutano na makundi ya wajasiriamali, bodaboda ambao wengi wao ni wazazi watarajiwa pamoja na wanafunzi katika shule za msingi na sekondari ilifanyika kwa lengo la kuitambulisha kampeni na namna ambavyo kila kundi litashiriki kwa nafasi yake.
Kampeni ya Lishe ya Mwanao Mafanikio yake iliyozinduliwa Disemba 22,2023 ,ni kampeni endelevu ambayo inafadhiliwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNICEF na USAID kupitia mradi wa lishe mtambuka.
Kauli mbiu ya Kampeni hiyo inasema “Kujaza Tumbo sio Lishe,Jali unachomlisha.”
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe