Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Njombe wamekutana katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika robo ya kwanza.
Akifungua Mkutano huo,Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Filoteus Mligo amewataka Madiwani kuhakikisha kuwa wanashiriki vyema katika ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kuwa mapato yanakusanywa kwa uhakikika kwani ndio muhimili mkuu wa uendeshaji wa Halmashauri.
Akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Afisa Tawala Wilaya ya Njombe Melkioni Kisinini amewataka Wananchi katika Wilaya ya Njombe kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Ebola ambao ni ugonjwa wa kutisha na umepoteza maisha ya Wananchi wengi katika Nchi za Jirani.
Kisinini aliendelea kusema kuwa Wilaya ya Njombe inampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendlea kuikumbuka Wilaya ya Njombe na kuiletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kutoa rai kwa Madiwani kuendelea kuisimamia kwa ukaribu miradi hiyo.
Wakichangia hoja katika Mkutano huo Madiwani wengi wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika Kata zao na pia wamesema kuwa ili kuunga mkono jitihada za Serikali ni vyema kuweka mkakati wa ujenzi wa nyumba za Waalimu ili kutatua changamoto za nyumba hizo hususani katika maeneo ya pembezoni.
Hoja nyingine iliyojadiliwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Wafanyabiashara mabao wanafanya biashara katika maeneo ambayo sio rasmi ambao tayari walishapatiwa maeneo ya kufanyia biashara kuhakikisha kuwa wanarudi katika maeneo hayo na kuacha kufanyia biashara kandokando ya barabara
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe