Halmashauri ya Mji Njombe Aprili 16, 2024 imepokea ugeni kutoka Halmashauri ya Mji wa Ifakara wenye lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo kilimo cha zao la parachichi.
Mafunzo mengine yamehusisha ukusanyaji na usimamizi wa vyanzo mbalimbali vya mapato, uendeshaji na usimamizi wa soko pamoja usafi na udhibiti wa taka ngumu.
Kiongozi wa msafara huo uliohusisha Waheshimiwa Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya ifakara Mhe. Kassim Faya Nakapala, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara amepongeza utendaji kazi wa Halmashauri ya Mji Njombe na namna ilivyoweka ubunifu katika ukusanyaji wa mapato.
Mhe. Kassim amesema, “tumefurahiswa na namna mapato yanayokusanywa yanarudishwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayowagusa wananchi moja kwa moja ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara.”
Halmashauri ya Mji Njombe hutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa barabara, asilimia 5 kwa ajili ya usafi wa mji na fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya ambapo kupitia mapato ya ndani halmashauri imeweza kujenga vituo vya afya vitano.
Kwa upande wake Thadei Luoga, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ameweka bayana vipaumbele vya Halmashauri kuwa ni, kutoa huduma bora kwa wananchi hasa katika upatikanaji wa huduma bora za ugani, afya na uhusiano mazuri kati ya wananchi na watumishi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
Katika hatuanyingine, timu kutoa Halmashauri ya Mji Ifakara ilimtembelea mkulima wa parachichi Mkoa wa Njombe Bwana Steven Mlimbila, maaraufu Nemes Green Garden kwa lengo la kujifunza kilimo cha parachichi yenye sifa na uhitaji mkubwa kwenye soko la dunia.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe