Wakipitia taarifa ya Kamati ya Uchumi baadhi ya Madiwani wameshauri ni vyema Idara ya Kilimo ikajikita katika kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya viwanda kwani Njombe inawakulima wa kutosha wa mazao mbalimbali changamoto kubwa ni ukosefu wa viwanda vya uchakataji.
Akizungumza wakati wa kujadili taarifa ya kilimo hususani kilimo Cha Parachichi Diwani wa Kata ya Makowo Edwin Mwanzinga amesema kuwa ni vyema shughuli uhamasishaji zikajikita katika kutafuta wawekezaji katika Sekta ya viwanda ili kuiongezea thamani Parachichi kwa kuhakikisha kuwa maparachichi yanayozalishwa hayaafirishwi kwenda nje na badala yake viwanda vinaanzishwa na uzalishaji wa bidhaa unafanyikia hapa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mheshimiwa Erasto Mpete ameunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa uhamasishaji katika Sekta ya viwanda ni jambo jema kwani litafungua milango kwa Wananchi kwa kujipatia ajira na pia kuongeza mapato ya Halmashauri ambayo yatatokana na mapato kupitia viwanda vitakavyokuwa vimeanzishwa ndani ya Hamashauri yetu
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe