Halmashauri ya Mji Njombe imeshika nafasi ya tatu katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nane nane Kitaifa.Katika maonesho hayo,Halmashauri ya Mji Njombe imeshika nafasi ya tatu kwa kumuibua Mfugaji bora wa Samaki Upendo Shari ambaye ufugaji wa samaki anaoufanya ni kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba na kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni nne.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji Njombe,Thadei Luoga amesema kuwa katika kipindi hiki mwamko wa Wadau umekuwa ni mkubwa ukilinganisha na vipindi vilivyopita ambapo hii imetokana na kuwa wengi wamekua wakiona faidi zitokanazo na maonesho hayo ndio maana wengi wamejitokeza kwa wingi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe