Halmashauri ya Mji Njombe imepokea madaktari bingwa sita (6) kupitia mpango wa madaktari bingwa wa mama samia, mpango unaolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa katika maeneo ya pembezoni na yenye uhitaji mkubwa wa huduma za afya.
Akizungumza Septemba 22, 2025 wakati wa mapokezi ya madaktari hao, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bi. Kuruthum Sadick, amesema kuwa uwepo wa madaktari bingwa unaenda kutatua changamoto za afya za wananchi huku akiwaomba wananchi kutumia fursa hiyo adhimu.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji njombe amempongeza Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi katika maeneo yao.
Madaktari hao watatoa huduma zifuatazo za magonjwa ya watoto , magonjwa ya ndani ,upasuaji ,magonjwa ya kinywa na meno ,usingizi na ganzi pamoja na huduma ya uuguzi.
Madaktari hao wanatarajiwa kutoa huduma kwa muda wa siku 4 kutoka Septemba 22 hadi septemba 26, wakiwa katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena).
Wananchi wote mnahimizwa kutumia fursa hii ya uwepo wa madaktari kwa kufika katika Hospitali ya Mji Njombe (Kibena) kupata huduma ambazo wengi walilazimika kuzifuata hospitali za nje ya Mkoa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe