Na.Ichikael Malisa.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa Tarehe 08 Novemba 2024 amepokea Matrekta 5 yaliyotolewa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Kituo cha zana za Kilimo kilichopo Halmashauri ya Mji Njombe Kata ya Lugenge kijiji cha Kisilo.
Akizungungumza baada yakupokea matrekta hayo Mhe.Kissa,ameeleza kuwa matrekta hayo yamefika kwa wakati muafaka kwa kuwa yatasaidia kuendeleza shughuli za kilimo na kuinua sekta ya kilimo kwa kuwasaidia wakulima vijana, na wanawake walioko kwenye mradi wa BBT (Building a Better Tomorrow) unatekelezwa katika Wilaya ya Njombe pamoja na wakulima wadogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zana hizo muhimu zitakazowasaidia wakulima kuondoana na changamoto za kilimo kwa kutumia jembe la mkono.
Halmashauri ya Mji Njombe imetenga maeneo kwa ajili ya Mradi wa BBT kwa Vijana na wanawake katika kata ya Makowo, Luponde, Utalingolo,na Lugenge.
Matrekta haya yatakuwa msaada mkubwa kwa wakulima kwa kuwa yatachangia kufanya kufanya kilimo cha kisasa kitakachoongheza uzalishaji wa mazao, hasa kwa vijana na wanawake ambao wanajihusisha na kilimo kama njia ya kujipatia kipato.
Pia zana hizi za kisasa ziasaidia kuwaondolea wakulima changamoto ya kutumia zana duni na njia za kilimo zisizo na tija, kwa kuwatengenezea mazingira bora na ya kisasa. Halmashauri ya Mji Njombe inatarajia kwamba msaada huu utasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, hivyo kuleta mabadiliko chanya katika mji huo na kuboresha hali ya maisha ya wakulima.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe