Tarehe 20 Desemba 2024 , Halmashauri ya Mji Njombe imepokea viongozi na wajumbe wa Chama cha Tawala za Mitaa (ALAT) Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Dkt. Salehe Mkwizu, kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kujifunza kuhusu ukusanyaji wa mapato na kilimo, hasa cha parachichi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Emmanuel Luhamba, akiwakaribisha wageni hao, alisema ziara hiyo ina faida kubwa kwa pande zote mbili, hususan katika kubadilishana uzoefu wa kilimo, kwani hali ya hewa ya Njombe na Kilimanjaro zinafanana kwa kiasi kikubwa.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, wajumbe hao walipata fursa ya kusikiliza mada mbalimbali zilizotolewa na Mweka Hazina na Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Njombe. Mada hizo zilihusu mbinu zilizotumika kuongeza mapato ya halmashauri na kufanya kilimo chenye tija cha parachichi na viazi.
Baadaye, ugeni huo ulitembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na stendi mpya ya mabasi na soko kuu la kisasa, miradi ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza mapato ya ndani ya halmashauri.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe