Septemba 30, 2024,Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imefanya ziara ya kujifunza katika Halmashauri ya Mji Njombe, ikiwa na lengo la kujifunza kuhusu kilimo cha parachichi.
Akizungumza baada ya kuupokea ugeni huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Erasto Mpete, aliwakaribisha nakuwaeleza umuhimu wa kilimo cha parachichi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe katika kuongeza mapato ya Mkoa.
Ameongeza kuwa zao hilo limeleta mwanga mkubwa wa kiuchumi kwa wananchi, na kuwataka wageni hao kutembelea mashamba ya wakulima waliofanikiwa ili kupata maarifa ya kina kuhusu kilimo hicho.
Kwa upande wake, Mhe. Rachel Nyangasi, Diwani wa Kata ya Chigelana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kujifunza hatua zote muhimu za ulimaji wa parachichi, kuanzia maandalizi ya mashamba hadi usimamizi wa kilimo na ufikiaji wa masoko.
Pia, aliongeza kuwa wanatarajia kupata mbinu bora za kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe