Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick, katika kikao cha kutathmini utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa Lishe kwa kipindi cha robo ya nne Aprili -Juni mwaka wa fefha 2023/2024 amesema, Halmashauri ya Mji Njombe kipitia kwa maafisa lishe,watendaji wa kata ,vijiji na mitaa itaendelea kutoa elimu ya lishe kwa wananchi ili kuhakisha kila kaya inazingatia lishe yenye makundi yote sita ya vyakula ili kutokomeza udumavu.
Aidha katika kupambana na mimba za utotoni ambazo zinachangia mabinti kiacha shule pamoja na utoro shuleni amesema Halmashauri kupitia kwa maafisa elimu kata inafanya ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha kila mtoto anayepaswa kuwepo shuleni anakwenda shule na kumaliza masomo yake sambamba na kuelimisha jamii umuhimu wa elimu haswa kwa mtoto wa kike.
Bi.Kuruthum ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali wanaofanya kazi na Halmashauri ya Mji Njombe katika kuhimiza lishe bora ili kupambana na udumavu akiwaahidi ushirikiano ili kufikia lengo la kutokomeza udumavu Mkoani Njombe.
Kutokana na changamoto ya hali duni ya Lishe inayopelekea udumavu kwa watoto ,Mkoa wa Njombe unaendelea na Kampeni ya kupambana udumavu ya Lishe ya Mwanao ,Mafanikio yake ,yenye kaulimbiu isemayo "Kujaza tumbo siyo Lishe jali unachomlisha", iliyozinduliwa Disemba 22,2023 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe .Anthony Mtaka ambapo Halmashauri ya Mji Njombe imepiga hatua na hali ya udumavu imepungua kutoka asilimia 45 mwaka 2022 hadi asilimia 42.4 mwaka 2024 hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo UNICEF na TFNC
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe