Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,vijana,Ajira na wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema waajiri wanatakiwa kutoa kipaumbele cha ajira kwa wenye ulemavu kwa asilimia 3 kwa mujibu wa sheria.
Amezungumza hayo Waziri Ndalichako wakati wa kilele Cha maadhimisho ya siku ya wasioona Fimbo nyeupe yaliyofanyika kitaifa Mkoani Njombe ambapo amesema Serikali itaendelea kuwashika mkono walemavu wote na ndio maana imekuwa na utaratibu wa kutoa mikopo ya asilimia 2 kwao kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na mahitaji mengine.
Awali mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema jitihada kubwa zimefanyika na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha hata watoto wenye ulemavu wanapata haki ya kupata elimu hivyo jamii isiwafiche watoto ndani.
Mwenyekiti wa chama Cha wasioona Tanzania TLB Omary Mpondelwa na Subira Shedangio Kaimu katibu mkuu Taifa chama hicho wameiomba Serikali kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu kwani hakuna aliyependa wala anayetamani kuwa mlemavu licha ya jitihada kubwa zinafanyika.
Kwa upande wao watu wasioona akiwemo Pascal Msigwa mwenyekiti wa TLB Mkoa wa Njombe na Nuru Awadh Mkurugenzi wa taasisi ya wanawake na wasichana wasioona Tanzania wamesema wangali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutengwa na kutotazamwa kwa karibu kama watu wengine.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe 2023 inasema ''Upatikanaji wa teknolojia Fikivu Katika ujenzi wa uchumi wa kidigitali ni mkombozi kwa mtu asiyeona na Taifa''.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe