• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Hekta 357.3 za ITOA zakabidhiwa Halmashauri ya Mji Njombe

Tarehe iliyowekwa: November 8th, 2019

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa hatma ya Mgogoro uliokuwa ukihusisha Bodi ya Wadhamini wa Chai Igominyi –Igominyi Tea Out grawers Association (ITOA) mara baada ya Ofisi ya Kabidhi Wasihi Mkuu inayosimamia  bodi za wadhamini  kufanya uchunguzi na kubaini uwepo wa migogoro  katika suala la udhamini  na utekelezaji wa  azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa mazao ya Kimkakati yanakuwa chini ya ushirika na sio  bodi za wadhamini, na kusababisha hekta 357.3 zilizokuwa zinamilikiwa na ITOA kukabidhiwa Halmashauri ya Mji Njombe.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson amesema kuwa Uchunguzi uliofanywa na timu ya Wataalamu  kutoka Ofisi ya Msajili Vyama vya Hiari, Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu Ofisi ya Mrajisi na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri imebaini kukiukwa kwa taratibu  kwa mujibu wa sheria zilizowamilikisha maeneo hayo.

“Lengo la mashamba waliyokabidhiwa ITOA ilikuwa ni kwa lengo la kuyaendeleza kupitia kilimo mkakati. Timu ya uchunguzi imebaini kuwa mashamba hayo hayakutumika kama yalivyokusudiwa. Yapo pia maelekezo ya Serikali yaliyotoewa kuwa Taasisi zote zinazojishughulisha na mazao ya kimkakati ikiwemo chai ziweze kujisajili kwenye vyama vya ushirika. Ofisi yangu imeelekeza kwamba mashamba hayo yarejeshwe kwenye Halmashauri ili iweze kupanga matumizi ambayo yatajielekeza katika  kuendeleza zao la chai ambalo ni zao la Kimkakati.”Alisema Emmy

Aidha Bi Emmy amesema kuwa yapo mambo ambayo kwa kushirikiana na taasisi yake yanatakiwa kutekelezwa ndani ya siku thelathini ili kufanikisha maelekezo yaliyotolewa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri alisema kuwa mgogoro wa ITOA ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinakabili wakulima wa chai kwa muda  mrefu na amepongeza kwa jitihada zilizochukuliwa kwani kwa sasa Mashamba hayo yatakuwa chini ya Mkurugenzi na wakulima wa chai kuendelea kunufaika na kuishukuru RITA kwa maamuzi yaliyofikiwa.
 

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe