Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Njombe Ndug. Justine Nusulupila amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Njombe kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka 4 kutoka mwaka 2021-2024.
Amezungumza hayo Disemba 20,2024 katika Mkutatano wa Uwasilishaji wa Utekelezaji Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo aliweza kuipongeza Halmashauri ya mji Njombe kwa namna ambayo Mkurugenzi na Madiwani ambavyo wamekuwa wakitekeleza Shughuli za maendeleo kwa uaminifu mkubwa pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo zimekuwa zikijitokeza .
"Kwa Moyo wote nimpongeze Mkurugenzi wa Halmashauri Mji Njombe ,Mwenyekiti wa Halmashauri na Wataalamu wote kwa mambo ambayo mmekuwa mkiyafanya ya utekelezaji wa miradi ya mendeleo katika Halmashauri , niombe endeleeni kufanya kazi kwa bidii na kutatua kero za wananchi kama tulivyo waahidi wananchi"
Alisema Nusulupila Mwenyekiti wa CCM Wilaya Njombe .
kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe. Deo Mwanyika amesema kwa mwaka 2021-2024 jumla ya shilingi Bilioni 27 kutoka katika Sekta ya Elimu ,Kilimo ,Miundombinu ya barabara na Mikipo ya Asilimia 10 ya vijana ,wanawake na walemavu vimeweza kutekelezwa katika Jimbo la Njombe mjini.
Akiendelea kuzungumza katika Mkutano huo Mbunge Deo Mwanyika ameweza kuchangia zaidi ya shilingi milioni 400 toka mfukoni mwake kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe